Kilimo cha Kahawa

Kilimo Cha Kahawa 

Na John Mabagala - Bwana Shamba

Jana nilimtembelea mkulima wa kahawa kijana wa miaka 28 . Ana shamba la ekari kumi likiwa na miti13,230 ya kahawa. Kwa mwaka jana alivuna wastani wa kilo moja (patchment) kwa kila mti na kuwa na jumla ya kg 13000 za kahawa. Kila kilo aliuza kwa wastani wa shilingi 4500 na kupata jumla ya shilingi milioni 58 na laki 5 (58500000). Shamba hili linatunzwa kwa mbolea za asili tu anazonunua kwa vijana wenzake walioanzisha biashara ya kuzalisha mbolea za asili (fuatilia post zijazo kuhusu biashara ya mbolea za asili). Mwaka huu pia anategemea kupata sio chini ya milioni 58. Kipato hicho ni kikubwa sana kwa mwaka. Hadithi hii itupe nguvu vijana wa kitanzania kuwekeza kwenye kilimo biashara. Si lazima kila mtu alime matikiti au nyanya. Kama unaweza kupata ardhi Kigoma, Mbeya, Ruvuma, Rukwa, Katavi Kagera unaweza kuwekeza kwenye kilimo cha kisasa cha kahawa na ukajitengenezea uhakika wa kipato kwako na familia yako huku ukitoa ajira kwa vijana wengine. Kahawa yenye ubora kamwe haiwezi kukosa soko. #kilimoNiSayansi#KilimoNiBiashara#

Kwa habari zaidi wasiliana na:

John Mabagala

https://web.facebook.com/john.mabagala

jmabagala@gmail.com

+255 784 828927 or +255 754 282448