Kilimo cha Tangawizi/ Ginger Farming

Mawasiliano na Mwandishi/Mkulima: regmundhunja@gmail.com 0753009397/0655009397

 • UTANGULIZI

Tangawizi ni aina ya zao la kiungo ambalo sehemu inayotumika ni tunguu (rhizome). Ambao huonekana kama mizizi ya mmea. Mmea huu kitaalamu huitwa zingiber officinale.

       Asili ya mmea huu sehemu za kitropiki za bara la Asia hasa nchi za china za india. Zao hili huzalishwa kwa wingi nchini Jamaica.

    Hapa nchini zao hili huweza kustawi katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Ruvuma, kigoma, Tanga, Morogoro, Pwani, Mbeya na Kilimanjaro.

 

 

 

 • MATUMIZI

Tangawizi hutumika kama kiungo katika kuongeza ladha, harufu na changamsha katika vinywaji (kama soda, juisi, vilevi n.k) na vyakula mbalimbali kama mikate, biskuti, keki, nyama za kusaga, n.k

   Hutumika pia katika viwanda vinavyotengeneza madawa mbalimbali kama dawa za meno, kikohozi, tumbo na muwasho wa ngozi n.k.

 

 • KILIMO CHA TANGAWIZI SONGEA MADABA

Madaba ipo mkoa wa Ruvuma, wilaya ya Songea vijijini, ipo njiani inapotokea Njombe kwenda Songea mjini hivyo kifupi inapatikana katikati ya Njombe na Songea. Iyo huifanya Madaba kuwa na hali ya Hewa mbili ile ya Njombe na Songea. Pia Madaba ina rutuba ya kutosha kuweza kuhimiri mazao mengi ya kibiashara kama kahawa, Tangawizi, Ufuta, Soya, Ulezi n.k na ya chakula kama Mahindi, Maharage, Mpunga n.k hustawi maeneo ya Madaba .

         Rejea kichwa cha habari, Tangawizi ilianzwa kulimwa Madaba kama moja ya zao la kibiashara mwaka 2013. Hivyo kuwapatia wakazi wengi wa madaba fursa hii ya kibiashara na kila mkazi asiye lima basi huwa na ndoto hii kuwa ‘’ili nitoke kimaisha basi nijitahidi nilime Tangawizi’’. Basi Tangawizi ni uti wa mgongo kwa mkazi wa Madaba.

       Fursa hii pia inakujia wewe pia mwananchi wa Tanzania popote ulipo, kwa kufuata ushauri na utaalamu wa wakazi wa Madaba pia unaweza kuwa na ndoto zile zile za ‘Tangawizi mkombozi’.

         Basi nami kama rafiki wa Tangawizi nimekuandalia ‘’ kiarticle’’ hiki basi ili nawe uweze kuwa rafiki ya Tangawizi pia.

      

 • TABIA YA MMEA

Kama nilivyodokeza hapo juu, mmea huu huvunwa kama Tunguu hivyo basi; hutambaa chini ya ardhi, wakati wa masika hutoa majani juu ya ardhi.

       Ingawa hadi sasa kitaalamu haijasibitishwa kuwa ni aina gani ya tangawizi hulimwa hapa Madaba. Wengine husema ni white Africa (Jamaica) na wengine husema cochin (flint). Ambazo ndio maarufu hapa nchini Tanzania.

       Kikubwa sio aina ya mmea bali uwezekano wa kustawi na kutoa matunda mazuri, aina hizi hutofautiana tu katika majani na ukubwa wa tunguu. Ambapo Jamaica ina rangi hafifu ya kahawia na tunguu fupi wakati cochin ina tuguu fupi zaidi lenye ngozi ya rangi iliyo kati ya kijivu na nyekundu.

 

 • HALI YA HEWA YA UDONGO

Zao hili hustawi katika maeneo yenye hali ya kitropiki, kutoka usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita 1500 au zaidi. Huitaji mvua kiasi cha mm.1200-1800 na joto la wastani wa nyuzi za sentigradi 20-25. Hustawi vyema katika udongo tifutifu wenye rutuba na usiotuwamisha maji.

 

 

 

 

 

 • UPANDAJI

Zao la tangawizi hupandwa kwa kutumia vipande vya tunguu vyenye kichipukizi kizuri angalau kimoja na huweza kukatwa katika urefu wa sm.2.5-5. Wakati mwingine, vichipukizi vinavyopatikana katika kumenya tangawizi huweza kuhifadhiwa na kutumika kwa kupanda. Kiasi cha kilo 800-1000 cha vipande vya tunguu huweza kutumika kwa kupanda katika hekari moja.

       Nafasi inayotumika kupanda ni kati ya sentimita.23-30 kwa 15-23 na kina cha sentimita.5-10 na mara nyingi hupandwa katika matuta. Baadhi ya mazao huweza kupandwa katika shamba la tangawizi ili kuweka kivuli chepesi ingawa si lazima kivuli kiwepo. Inashauriwa kumwagilia maji endapo mvua inakosekana.

       Wiki 1-2 kabla ya kupanda weka mbolea ya samadi au mboji kiasi cha tani 4-8 kwa hekari na kwa kukuzia weka kiasi cha NPK kwa uwiano wa kilo 36:36:80. Tandaza nyasi shambani kuhifadhi unyevunyevu hasa pale kivuli kinapokosekana.

     Palizi hufanywa mara magugu yanapoota, na kawaida ni mara nne (4) wakati huo katika palizi ya tatu na ya nne hushauliwa kupandishia udongo kwa kila china la mmea ili kuupa mmea nafasi ya kutoa tunguu kubwa na nene

       Pia dawa ya kuuwa wadudu kama simazine hutumika.

 

 • MAGONJWA NA WADUDU
 • Madoa ya majani yanayosababishwa na

viini vya magonjwa viitwavyo

Colletotrichum zingiberisna Phyllosticta

zingiberi.

 • Kuoza kwa tunguu; kunasababishwa na

viini viitwavyo Pithium spp.

 • Mizizi fundo; inasababishwa na viini viitwavyo meloidegyne spp.

 

 • UVUNAJI

Tangawizi huweza kuwa tayari kwa kuvuna kati ya miezi 9-10 baada ya kupanda, wakati majani yake yanapogeuka rangi kuwa njano na mashina kusinyaa. Tangawizi inayohitajika kwa kuhifadhi kwenye kemikali (preserved ginger in brine) huvunwa kabla haijakomaa kabisa, wakati ile iliyokomaa kabisa huwa kali zaidi na huwa na nyuzi hivyo hufaa kwa kukausha na kusaga. Mavuno hutofautiana

kulinganana na huduma ya zao, mavuno yanaweza kuwa kiasi cha tani 8-12 cha

tangawizi mbichi huweza kupatikana.

 

 • USINDIKAJI

Tangawizi ikisindikwa utapata unga, mafuta maalum (essential oils) n.k. Tangawizi iliyovunwa huweza kumenywa, kukatwa na kukaushwa juani au mara nyingine huchovywa katika maji yaliyochemka kwanza na ndipo kukaushwa au hukamuliwa mafuta. Pia tangawizi husindikwa na kuhifadhiwa kwenye chupa zikiwa zimechanganywa na sukari na/au chumvi. Hata hivyo tangawizi ina Kiasi cha mafuta cha 16%-18%.

 • SOKO LA TANGAWIZI

Soko la Tangawizi lipo ndani na nje ya nchi, Hapa nchini huuzwa kwa bei ya Tshs. 2000-4000/= `kutegemea na msimu.

 

 • GHARAMA ZA UZALISHAJI NA MAPATO

         Gharama ya hekari moja

Kukodi shamba                         Tshs.         100,000/=

Mbegu                                                           2000, 000/=

Kulima                                                                100,000/=

Kupanda                                                              100,000/=

Kupalilia                                          4                 360,000/=

Mbolea / samadi                                                 150,000/=

Jumla                                                                     2,810,000 /=  

 

               Mapato kwa hekari moja      

kilo                                               &nbs